Je utajiri wa Elon Musk unaweza kuinunua Apple?
Hapana, licha ya Elon Musk kuwa ndiye tajiri namba moja duniani akiwa na utajiri mkubwa mno wa $220 Bilioni unaoweza kununua makampuni makubwa mbalimbali na hata kushinda bajeti za miaka kadhaa za baadhi ya nchi lakini hawezi kuimiliki kampuni yote ya apple ambayo ina thamani ya zaidi ya $2 Trilioni, kama Elon Musk atatumia utajiri wake wote basi atamiliki 8% tu ya shares zote za kampuni ya apple, hata CEO mkuu wa sasa wa Apple Tim Cook ana share ya 0.02% tu ya kampuni hiyo ( 🖋️ Hashim Seki)
Tags
Je Wajua