-Ikiwa utauliza je jina Tanzania limetokea wapi au limetungwa na nani? basi usishangae kupata majibu mengi yatakayo kuchanganya. Basi leo ngoja nikujulishe historia fupi ya jina hili la nchi yetu ili wote tuwe na jibu moja sahihi.
-Jina la Tanzania linatokea karibu kabisa na milima ya Uluguru wilayani Mvomero katika mji wa Morogoro, pale kijana wa miaka 18 katika shule ya sekondari mzumbe alipoona tangazo la wizara ya habari na utalii katika gazeti la "The standard" juu ya uhitaji wa jina la muungano wa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.
-Kijana huyo aitwaye Mohammed Iqbal Dar aliunganisha herufi tatu(3) za kwanza za Tanganyika na Zanzibar yaani Tan+Zan =Tanzan kisha kumalizia na neno "ia" (Tanzan-ia) kwa kuwa nchi nyingi za Africa pia ziliishia na "ia" kama vile Zambia, Liberia, Namibia, Somalia,Tunisia n.k basi baada ya kuandika akatuma barua yake wizara ya utalii na habari na huo ndio ukawa mwanzo wa jina la thamani la TANZANIA.
-Mohammed Iqbal Dar hakuwa mtu pekee aliyetunga jina hili bali Kuna wenzake wengine 15 ambao hawakutokea siku ya kutoa zawadi katika hafla iliyoandaliwa na wizara ya habari na utalii. Hivyo yeye pekee ndiye anaetambulika kama muasisi wa jina la TANZANIA na alizawadiwa Tsh 200 kama pongezi! (Tsh 200 ya miaka ya 60 sio sawa na Tsh 200 ya sasa ya kupanda daladala kwa wanafunzi).
-Kwa sasa Mohammed Iqbal Dar anaishi Birmingham Uingereza na ni muhandisi wa masuala ya redio na huko nyumba yake ameiita Dares salaam.
Muandishi: Luqman Kisokora
Mhariri & Msomaji: hashim_seki
Publisher:
YouTube: 99 TZ | ©2021