Lupita Nyong'o Ndani Ya Filamu Ijayo Ya A QUIET PLACE

Muendelezo wa filamu za A QUIET PLACE unatarajiwa kutoka mnamo tarehe 08 . 03 . 2024 ambapo itakuwa ni filamu ya tatu kwenye mfululizo huo na inaitwa A QUIET PLACE : DAY ONE .

Ndani kutakuwa na waigizaji maarufu kama vile Lupita Nyong'o ambaye ameigiza kama Mama anayepambana kuilinda familia yake dhidi ya viumbe hatari [ Aliens ] ambayo wanaua kwa kusikia sauti . Pia kuna Muigizaji kama Joseph Quinn ambaye amepata sana umaarufu kwenye Series ya THE STRANGER THINGS bila ya kuwasahau Alex Wolff Na Djimon Hounsou .

Kwenye filamu hii tutaona zaidi matukio ya mwanzoni kabisa pale Aliens hapo walipovamia dunia na kuanza kufanya uharibifu na mauaji makubwa , huku wakiwa na uwezo mkubwa wa kutambua sauti na kuifata inapotokea na kwenda kufanya mauaji  .

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form