Mambo 7 Usiyoyajua Kuhusu Viatu Vya Air Jordan

Unapozungumzia mpira hutoacha kutaja jina la Ronaldo Au Messi , na hata Unapozungumzia viatu hutoacha kutaja Air Jordans . Hivi ni moja ya viatu maarufu sana duniani ambavyo kwa mwaka 2022 , Jordan brand imeingiza zaidi ya $5.1B [ Shilingi Trilioni 12 .11 Za Kitanzania] Lengo hapa sio kuzungumzia mapato ya brand ya Jordan bali nitakuketea mambo 7 muhimu ambayo kama mvaaji au mdau  wa viatu , ni vizuri kuyajua  .

1. Kiatu cha kwanza kabisa cha Air Jordan kilitengenezwa mnamo mwezi wa kumi mwaka 1984 na kuingia rasmi sokoni tarehe 01 . 04 . 1985.


2 . Air Jordan 1 alizokuwa anavaa Jordan kwa mara ya kwanza zilikuwa na rangi nyekundu na nyeusi .Viatu hivyo vilikiuka sheria ya NBA ya wakati huo ambayo ilitaka viatu vya Wachezaji viwe na 51% ya rangi nyeupe .Kushindwa kufanya hivyo kutapelekea kupigwa faini ya USD 5,000 [ $1,497 ( Takribani Milioni 33 kwa sasa ) ] kwa kila mechi . Air Jordan 1 ilikuwa na 23% ya rangi nyeupe tuu ,Hivyo Nike walikubali kutoa fine hiyo ili Michael Jordan aendelee kuvaa viatu hivyo .

Barua Kutoka NBA Ikimuonya Jordan Kuhusu Viatu Vyake Vilivyokuwa Vinakiuka Sheria Za NBA 


3 . Kuna msemo unasema " Fursa ni changamoto zinazokuzunguka " , basi Nike wakatumia fursa ya kupigwa marufuku kwa viatu vya  Air Jordan 1 kutangaza biashara yao na Tangazo lilisomeka " "On Oct. 15, Nike created a revolutionary new basketball shoe. On Oct. 18, the NBA threw them out of the game. Fortunately, the NBA can't keep you from wearing them. Air Jordans. From Nike." . likimaanisha kuwa " Nike imetengeneza kiatu cha Air Jordan 1 , lakini NBA wamekufungia .. hii haikuzuii wewe kuacha kuvaa kiatu cha Air Jordan " ... Tangazo hilo liliuza sana na kuingeza umaaarufu wa viatu hivyo .


 4 .Bei ya kwanza ya Air Jordan 1 ilikuwa ni $65 [ sawa na $183 kwasasa  [ 435 , 000 za kitanzania] .

5 . Kampuni ya Nike ilitegemea kuingiza $3M ndani ya miaka mitatu . Waswahili wanasema kizuri chajiuza , kibaya chajitembeza . Ndani ya mwaka mmoja tuu iliingiza takribani $126M. 


6 . Logo ya Jumpman ilitokana pale designer wa Peter Moore alipoona pozi la Michael Jordan kwenye Life Magazine [ Gazeti la Life ] iliyopigwa mwaka 1984 kwa ajili ya Mashindano ya Olympic .

Michael Jordan Mbele Ya Gazeti, Ambapo Moore Alipata Wazo La Jumpman 

Moore aliingia studio mwaka 1985 na Jordan na kutengeneza pozi kama hilo kwa ajili ya Nike .

Michael Jordan Akiwa Studio Kwenye Kutengeneza Logo Ya Jumpman 

Hatimaye mwaka 1988 , designer TINKER HALTFIELD alichora mchoro huo wa Jumpman kupitia wazo la designer mwenzake wa Nike , yaani  Peter Moore.

Logo Ya Jumpman Iliyochorwa Na Tinker Haltfield


7. Kiatu cha kwanza chenye Logo ya Jumpman ni Air Jordan 3 ambacho kilivaliwa tarehe 27 . 01 . 1988 .

Michael Jordan Aliyekalia Mpira Akiwa Amevaa Air Jordan 3 Yenye Logo Ya Jumpman 


Ukiachana na hayo mambo 7 muhimu ya kiatu cha Air Jordan , pia tukirudi kwa Michael Jordan , inakadiriwa kuwa kwa mwaka 2022 pekee kampuni ya Nike ilimpa zaidi ya $150M+ [ Shilingi Bilioni 356 Za Kitanzania ] kutokana na mkataba wao walioingia toka mwaka 1984 .

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form