Asilimia kubwa ya watu wanakula korosho kwa kiwango kikubwa wamekuwa wakilalamikia maumivu ya tumbo , tumbo kujaa gesi na wengine hadi kuharisha kabisa . Je unafahamu sababu inayopelekea hali hiyo ?
Korosho zina aina ya kichocheo kiitwacho PHYTATES ambacho kazi yake ni kutunza madini muhimu kwenye mbegu za korosho na kuja kuyaachia pale mbegu inapoanza kuota , lengo likiwa ni kuipa mbegu mahitaji muhimu pale inapohitaji ili iweze kutoa kuwa mmea
Kichocheo hicho kipo kwenye kila mbegu ya Korosho hivyo unapokula Korosho , Kichocheo huingia kwenye mmeng'enyo wako wa chakula , Wahenga wanasema hakuna binadamu mkamilifu . Kwa bahati mbaya binadamu hatuna kimeng'enya cha PHYTASE ambacho kazi yake ni kuvunja vunja ( kumeng'enya )PHYTATES .
Kutokana na hali hiyo PHYTATES haiwezi kumeng'enywa ndani ya mfumo wa mmeng'enyo na huweza kushikilia( bind ) baadhi ya madini muhimu kwenye mmeng'enyo wa chakula , hivyo kupelekea vimeng'enya kupunguza kufanya kazi kwa ufanisi . Kutokana na vimeng'enya kutofanya kazi kwa ufanisi , hali hii hupelekea mfumo wote wa mmeng'enyo wa chakula kushindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa hivyo mtu huweza kujisikia hali ya tumbo kuuma , kujaa gesi na hata kuharisha pale zinapoliwa kwa kiwango kikubwa .
NJIA ZA KUPUNGUZA ATHARI HIZO .
Dalili hizo sio za kudumu na huisha baada ya muda fulani . Pia kuna baadhi ya njia za kupunguza dalili hizo ambazo ni :
1 . Kula korosho kwa kiasi ( kiwango cha kawaida )
2 . Kuziloweka korosho zako kisha kuzikausha . ( unapoloweka korosho Mbegu inatambua kuwa muda wa kuota ni tayari , hivyo PHYTASE huanza kuivunja PHYTATES , hivyo kuondoa hizo athari pale inapoliwa ).
FAIDA ZA KOROSHO MWILINI
Licha ya athari hizo Korosho zina faida nyingi mwilini na inashauriwa ziliwe kwa kiasi . Mojawapo ya faida hizo ni :
1 . Kuboresha kiwango cha sukari mwilini kwa kuwa Korosho zina kiwango kidogo cha sukari .
2 . Ina Nyuzi nyuzi ( fibers ) muhimu kwa ajili ya mmeng'enyo wa chakula
3 . Kuboresha mzunguko wa damu kwa kuwa zina madini ya Magnesium, Copper n.k
4 . Kuboresha afya ya Moyo kwa kuwa zina kiwango kidogo cha mafuta . Hivyo kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya Magonjwa ya Moyo .
5 . Korosho zina protini, wanga na mafuta hivyo ni nzuri kwenye kuboresha afya ya mwili kwa ujumla .
6 . Kupunguza athari za maambukizi ( inflammation) kwa kuwa Korosho ni antioxidant
Source : Havard Public Health