Mwaka 1974 ulikuwa ni mwaka wa majonzi kwa mashabiki wa timu ya Manchester United na pia historia iliandikwa kutokana na timu hiyo kushuka daraja huku wakifungwa goli 1 - 0 dhidi ya Wapinzani wao ambao ni Manchester City katika mechi ya mwisho na ikawa ya timu ya 21 kati ya 22 zukizokuwa zinashirika ligi kuu nchini Uingereza . Lakini maajabu ni kuwa tukio hilo halikudumu sana kwenye vinywa vya wanamichezo kwa sababu miezi 6 mbele , dunia nzima inakuja kuzungumzia tukio la kihistoria kwenye ulimwengu wa michezo .
Unataka kufahamu nini mpaka kilifanya mpaka kushuka kwa Manchester United kusiiteke dunia kwenye ulimwengu wa michezo ? .
Basi huko Kinshasa , Zaire [ Congo ] kuna tukio kubwa lililoisimamisha dunia lilikuwa linaenda kutokea .Ni THE RUMBLE IN THE JUNGLE " lilikuwa ni jina la pambano kali baina ya Muhammad Ali [ 32 ] na George Foreman [ 25 ] . Kwa bara la Afrika lilikuwa ni pambano kubwa na la kwanza kwa Mabondia Wa Uzito Wa Juu [ Heavy weight championship ] huku promoter ni mmarekani ambaye ni Don King , usichokijua ni kuwa hao wote ni weusi .
Don King alikuwa promoter mweusi anayetafuta wadhamini kwenye kuandaa pambano hilo , lakini hakufanikuwa kwa kuwa kipindi hicho , kwa kuwa ilikuwa ni ngumu kwa mtu mweusi kuandaa Pambano huko Marekani , na sehemu kadhaa alipoenda alikatishwaa tamaa kwa kuambiwa haitowezekana . Lakini licha ya changamoto hizo Don aliwasainisha mkataba Mohammed na George ambapo kila mmoja angepata kiasi cha $5M [ ambapo kwa sasa ni takribani $32M ambazo ni sawa na zaidi ya Bilioni 70 za kitanzania ]kama watapambana kwenye pambano lake , yaani Don aliamua "kujilipua " kama vijana wa sasa wanavyosema . Pia mkataba huo ulisaidia kufanya hata mapromoter wengine washindwe kuandaa pambano baina ya watu hao kipindi hicho kwa kuwa waliwekewa pesa nyingi na Don . Hivyo Don akabaki na kazi moja tuu ya kuanza kutafuta wadhamini nje ya Marekani.
" Ukiona giza nene , jua asubuhi inakaribia " haya maneno yanatokea kwa Don King kwani baada ya jitihada kadhaa hatimaye Fred Weymar Mmarekani ambaye alikuwa ni mshauri wa Raisi Mobutu Sese seko wa Zaire , alimshauri Mobutu kudhamini pambano hilo kwa kuwa lingesaidia utawala wake na kutangaza nchi yake zaidi . Hatimaye Mobutu akakubali kudhamini pambano hilo na kuamua lifanyikie Zaire [ Congo ].
Rais Wa Zaire Mobutu Mwenye Kofia , Kushoto Kwake Ni Muhammad Ali Na Kulia Ni Promoter Don King |
Pambano hilo mara ya kwanza liliitwa " From The Slave Ship To Chhampionship " likimaanisha kuwa Ali na George wote wana asili ya Afrika na babu zao walikuwa watumwa na sasa wanarudi nyumbani kama mabingwa , lakini baadaye jina hilo lilibadilishwa kwa kuona kuwa jina hilo lingewagawa mashabiki wa mchezo huo na hatimaye walikiita " The Rumble In The Jungle " likimaanisha Muungurumo ndani ya msitu , ambapo wanaume wawili wanapambana ndani ya ardhi yenye msitu mkubwa ya Zaire [ Congo ]
Pambano hilo lilipangwa kufanyika 25 . 09 . 1974 huko Kinshasa , Zaire lakini kwa bahati mbaya George Foreman aliumia mazoezini na kupasuka juu ya jicho lake la kulia , hali hiyo ilipelekea Pambano kusogezwa mbele kwa takribani wiki tano [ 5 ] mpaka 30 . 10 . 1974 na George akishonwa nyuzi 11 kwenye kidonda chake .
Waswahili wanasema " hayawi hawayi yammekuwa " , hatimaye mnamo saa 10 na 30 alfajiri , Watu takribani 60,000 walikusanyika kwenye uwanja wa Stade de 20 Mai kushuhudia pambano lililoteka hisia za watu wengi kipindi hicho na Dunia kwa ujumla , Inasemekana ni pambano lililotazamwa na takribani watu Bilioni 1 duniani takribani robo ya idadi ya watu wote duniani Wakuokuwa Bilioni 4 wakati huo [ 1974 ].Pambano hilo lililokuwa linafanyika huko Kinshasa , nchini Zaire [ kwasasa ni Congo ] lakini dunia nzima ilisimama kuwatazama Muhammad Ali [ 32 ] na George Foreman [ 25 ] wote raia wa Marekani ndani ya Congo , Afrika wakipigania mkanda wa Uzito wa Juu Wa Masumbwi .
Mohammed Ali akisifika kwa ufundi na ustadi wa hali ya juu kwenye mapambano yake , huku George Foreman akisifika kwa nguvu na ngumi nzito .
Uwanja mzima ulikuwa unamshangilia Mohammed Ali wakiimba " Ali , bomaye " wakimaanisha " Ali , muue huyo " .Muhammad Ali alishangiliwa sana kutokana na rekodi zake alizokuwa nazo huko nyuma lakini pia aliitumia mbinu ya kumwita George kama Mbelgiji kwa kuwa watu wa Zaire [ Congo ] waliokuwa wametawaliwa na Wabelgiji , hivyo walikuwa na chuki nao . Na Ali alitumia fursa hiyo kujiongezea mashabiki lukuki .
Muhammad Ali Akishangiliwa Na Wananchi Wa Zaire Kabla Ya Pambano |
Baada ya kengele kulia tuu , basi George alianza kumshambulia kwa kasi na nguvu zote , lakini Muhammad Ali alijibana kwenye kamba huku akikwepa kwa ufundi na ustadi wa hali ya juu makonde yote ya George [ hiyo style alliita rope-a-dope ] ambaye alikuwa anashambulia kama Faru aliyejeruhiwa .
Mvumilivu hula mbivu , hii ndiyo mbinu aliyoitumia Ali .Ali alijua udhaifu wa mpinzani wake , hivyo alimsubiri azidi kutumia nguvu zake na pale atakapochoka aanze kumrudia yeye .
Baada ya round ya 5 , George alianza kuchoka huku hasira zikimzidi kwa kuwa kila alichokuwa akifanya kilikuwa hakifanikiwi , alishindwa kuvumilia , na kuzidi kufura , Muhammad Ali akiendelea kumdokoa kwa ngumi kadhaa za uso huku akiweka guard kali na George kushindwa kumlenga Ali usoni.
Mapumziko kabla ya round ya 6 , Boxing official kutoka Zaire alienda kulegeza kamba za ulingo na kufanya kamba zilegee , Dundee ambaye ni mwalimu wa Muhammad Ali alimuelekeza kutoegemea tena kamba kwani ingepelekea kuanguka kutoka ulingoni kwa kuwa zikikuwa zinekegezwa , Ali alitoka kwenye kamba na kuanza kumshanvukia George kwa kasi huku akimkwepa na kumkimbia , hali iliyozidi kumchosha George.
Muhammad Ali Akiwa Kwenye Kamba Akikwepa Ngumi Za George Kwa Ufundi Wa Hali Ya Juu [ rope-a-dope ] |
Ilipofika round ya 7 , George alifanikiwa Ä·umpiga hali ngumi nzito kwenye jaw , lakini Ali alimnong'oneza George na kumwambia " That all you got , George ? " akimaanisha kwamba huo ndiyo uwezo wako ulipoishia hapo George? . Hali hii ikizidi kumtia hasira George na kumtoa mchezoni kiakili . Pengine alipokosea George ni kuingia kwa kujiamini kwa hali ya juu na kutaka kumpiga Ali KO round za mwanzoni .
Ilipofika round ya 8 , Ali akaiona fursa na haraka kwa wepesi wa hali ya juu akatoka kwenye kamba ipokuwa akuzuia ngumi za George na kuanza kumshambulia usoni , hatimaye George alipoteza balance huku miguu yake ikitepeta akadondoka chini akiwa hoi.
Hatimaye Muhammad Ali alishinda pambano hilo huku George Foreman likiwa ni pambano lake la kwanza kupoteza katika mapambano yake 40 aliyopambana mpaka muda huo [ kwa mara ya kwanza anapigwa na Mohammed Ali ] .
George Foreman akidondoka baada ya kupigwa KO na Muhammad Ali |
Rekodi
Pambano hilo liliangaliwa na Waingereza takribani Milioni 26 kupitia BBC One ikiwa ni takribani nusu ya raia wote wa Uingereza ambao walikuwa ni Milioni 56 wakati huo .
Pia Pambano hilo linakadiriwa kuingiza takribani USD 100M [ kwa thamani ya sasa ni USD 600M ( Ambazo ni sawa na Shilingi Trilioni 1.42 za kitanzania) ] .
Pambano hilo linabaki kuwa moja ya mapambano ya kihistoria kuwahi kutokea duniani .THE RUMBLE IN THE JUNGLE , na hatimaye Mohammed Ali anarudisha heshima yake kwa kumpiga bondia ambaye hakuwahi kupigwa kwa mapambano yote 40 .
Maisha Baada Ya Pambano.
Muhammad Ali na George Foreman walibaki kuwa marafiki wa karibu baada ya pambano hilo . Na hata pale mwaka 1996 kwenye jukwaa la Oscars kwenda kupokea tuzo ya filamu ya When We Were Kings [ inayohusu pambano la The Rumble In The Jungle] , George alimsaidia Ali kupanda jukwani kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa ugonjwa wa Parkinson [ ugonjwa unaoathiri mfumo wa fahamu na mijongeo ya mwili ].
George Foreman |
Kwa sasa George Foreman ana umri wa miaka 74 ,Wakati Muhammad Ali hatunaye tena duniani na alifariki mnamo tarehe 03 . 06 . 2016 akiwa na umri wa miaka 74 .