Je Unafahamu Kuhusu Wanyama Wanaofanana Na Majani ?

Ushawahi kupita porini na kuona jani linatembea ? Na ukafikiri kuwa ni jani linapelekwa na upepo ? .Basi baada ya makala hii utakuwa na majibu mawili , yaani linaweza kuwa Jani au Mdudu . Ndiyo ni Mdudu .

Basi leo niazime muda wako kidogo nikueleze kuhusu Mdudu Jani ( Leaf Insect ) yaani ni Mdudu mwenye umbo kama la Jani .Wadudu hawa wanatokea kwenye familia ya Phylliidae ( Phyllidae family ) kutoka kwenye kundi la wanyama ( Animal Kingdom ) na kuna zaidi ya aina 50 za Wadudu hao ( 50 Species) .

Kwa Wadudu hawa Mwanamke ni Mkubwa Kuliko Mwanaume na Urefu wa miili yao huwa kati ya Sentimita 2 mpaka sentimita 10 .Pia huzaliana kwa kutaga mayai kama Wadudu wengine Na baada ya kutotolewa huwa na rangi nyekundu hivi na hupanda juu ya miti kula majani ambapo baadae huwa na rangi ya kijani .Viumbe hawa ni adimu na huwa wanapatikana sana Australia Na Asia ya Kusini .

Inaaminika kuwa Msomi Antonio Pigafetta karne ya 16 ndiye mtu wa kwanza kutoka Ulaya , aliyeandika na kuchapisha kuhusu Wadudu hao .

" In this island are also found certain trees, the leaves of which, when they fall, are animated, and walk. They are like the leaves of the mulberry tree, but not so long; they have the leaf stalk short and pointed, and near the leaf stalk they have on each side two feet. If they are touched they escape, but if crushed they do not give out blood. I kept one for nine days in a box. When I opened it the leaf went round the box. I believe they live upon air " ,

 Akimaanisha kuwa kwenye kisiwa hicho amekutana na majani ambayo yanatembea baada ya kudondoka kutoka mitini na ukutaka kuyagusa hukumbia na kujihanganya kwenye majani na pia anaongezea kuwa hata ukiwakanyanga hayatoi damu . Aliongeza kuwa Majani hayo yana miguu .


NJIA YA KUISHI WADUDU HAO 

Umbo linalofanana na jani lililong'atwa linamsaidia vizuri kujificha kwa maadui zake , kwani jani lililong'atwa huchukuliwa kama halina mvuto tena .

Mwendo wake ni kama jani linaloanguka kutoka juu ya mti huku likupulizwa na upepo mwanana na wenye kasi ndogo na hii pia huzidi kuwachanganya maadai zake maradufu , kwa kudhani ni jani linalopeoerushwa na upepo tuu .

Waswahili wanasema kua uyaone na dunia kila siku itakushangaza .Basi kuanzia leo tujue kuwa tuna wanyama wenzetu ambao wanafanana kama majani ( kisayansi wote tunatokea kwenye kundi la Wanyama [ animal kingdom ] )

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form