Mnamo tarehe 20 . 05 . 1997 huko Kanagawa , Japan anazaliwa kijana wa kijapani ambaye miaka 25 mbele anakuja kutoa assist ya ajabu kwenye kombe la dunia la mwaka 2022 kwenye mechi dhidi ya HISPANIA nchini Qatar na kuipeleka JAPAN hatua ya 16 bora . Kijana huyo ni KAORU MITOMA ( 25 ) ambaye kwa sasa anacheza nafasi ya Winga ndani klabu ya BRIGHTON & HOVE ALBION inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza .
Baada ya mwaka 1997 twende miaka 19 mbele ambapo ndipo kwenye lengo la makala hii .Ilikuwa ni mwaka 2016 ambapo MITOMA alipata ofa ya kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya KAWASAKI FRONATALE huko kwao japan lakini kijana mwenye mwenye umri wa miaka 18 kipindi hicho alikataa ofa hiyo na kuamua kwenda chuo cha utafiti nchini humo kiitwacho TSUKUBA kwa miaka ambapo alisomea NJIA ZA KISAYANSI KWENYE MAZOEZI , LISHE , UKOCHA n.k .
Kuhusu maamuzi hayo mchezaji alisema " Nafikiri ni vizuri nikienda chuo ili kuja kuwa mchezaji wa soka la kulipwa " na kuongezea kuwa " Chuoni nimejifunza Mazoezi , Lishe , Ukocha na vitu vingine vingi " .MITOMA aliona ni vizuri kwenda chuo na kujifunza zaidi kama ya kuwa Mchezaji wa kulipwa.
Akiwa chuoni akiamua kuanza kufanya utafiti kuhusu dribbling , MITOMA alijifunga kamera kichwani mwake na kuanza kurekodi mijongeo yake yote akiwa na mpira na kuangalia kwa makini mijongeo ya mpinzani wake na kisha usiku alikuwa akisoma taarifa alizokusanya kwenye kompyuta yake .
MITOMA akimalizia utafiti wake alikuja kugundua kuwa ili ufanye vizuri kwenye dribbling ni lazima Umuangalie mpinzani wako na nafasi iliyopo mbele yako kabla ya kuchukua mpira na baada ya kupata mpira inabidi uanze kukimbia kwa kutazama mbele bila ya kuangalia chini huku akichezesha mwili wako kidogo ili kupoteza balansi ya mpinzani wako .Pia aligundua kuwa inatakiwa uwe ubabadili kasi yako na kumdanganya mpinzani wako ili kujitengenezea nafasi .
Utafiti wake huo umewekwa chuoni hapo na wanafunzi mbalimbali hufundishwa kupitia kazi hiyo ya MITOMA .Akiwa chuoni alijifunza jinsi ya kusprint kutoka kwa TONOGAWA ( Aliyekuwa muwakilishi wa Japan katika Olympics 2000 mpaka 2004 ) , jinsi ya kukimbia kwenye mstari ulionyooka kupitia kocha wake wa mazoezi na pia alimwambia Mtaalamu wa Lishe kumuandalia chakula maalumu kwa ajili ya kuongeza nguvu na afya yake .
Aliingia mkataba na KAWASAKI mwaka 2018 na kuanza kuitumikia klabu hiyo mwaka 2020 ambapo msimu wa kwanza hapo KAWASAKI alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12 za magoli kwenye mechi 30 .
Akafanikiwa kujiunga na BRIGHTON & HOVE ALBION mnamo tarehe 10 . 08 . 2021 .
Baada ya hapo yaliyofuata ni makubwa mno ukitaka kujua makubwa yake kawaulize UJERUMANI kule Qatar bila ya kuwasahau HISPANIA, Baada ya kutoka Qatar njoo ulaya ndani ya nchi ya Uingereza halafu piga stori mbili tatu na mabeki wa timu pinzani kuhusu Mwamba huyo wa kijapani na watakupa habari zake . Kwenye hao mabeki usisahau kuwauliza mabeki wa Arsenal na Liverpool. ( 🖊 Luqman Kisokora )