Filamu ya FAST X ni filamu ya 10 kwenye Mfululizo wa filamu za FAST AND FURIOUS , Ambapo tunarudishwa nyuma mpaka mwaka 2011 kwenye FAST AND FURIOUS 5 kipindi ambacho DOM ( VIN DIESEL ) pamoja na kundi lake walifanya mission huko Brazil na kufanikiwa kumteketeza Bosi wa madawa ya kulevya aitwaye HERNAN REYES na kuangamiza himaya yake yote . Miaka 12 inapita na Mtoto wa Reyes ambaye ni DANTE ( JASON MOMOA ) anakuja kulipiza kisasi kwa hasira na uchungu mkubwa huku shabaha yake ni DOM na watu wake wa karibu . Hivyo DOM na kundi lake wanajikuta wakiwa wanashambuliwa na pande mbili yaani huku CIPHER huku DANTE .
Tags
Movies