Tanzania Yaingiza Timu 2 Kwenye 20 Bora Afrika . Simba Ikiwa Ya 7 Na Yanga Ya 16

Mashindano ya vilabu vya Afrika yalitamatika rasmi mwezi wa sita ( June ) .
Huku Mashindano ya Shirikisho [ CAF CONFEDERATION CUP ] yakitamatika tarehe 03 . 06 . 2023 kwa USM Alger kuchukua kombe mbele ya Timu pekee kutoka Afrika Mashariki na Tanzania kwa ujumla , yaani Young Africans . Upande wa klabu bingwa Afrika [ CAF CHAMPIONS LEAGUE ] Fainali ya pili kati ya Wydad Casablanca Dhidi ya Al Ahly ilitamatika 11 . 06 . 2023 kwa Al Ahly kubeba Ubingwa huo. 

Baada ya kutamatika kwa Mashindano hayo, CAF huzipa kila timu Alama kulingana na viwango vilivyooneshwa na timu husika kwa kipindi cha miaka mitano. Kwa msimu wa 2023-2024 . Viwango vya timu na alama zao ni kama zifuatazo ;

 1 . Al-Ahly [ Misri ] = 57

2 . Wydad AC [ Morocco ] = 50

3 . Espérance de Tunis [ Tunisia ] = 36

4 . Raja Casablanca [ Morocco ] = 35

5 . Mamelodi Sundowns [ Afrika Kusini ] = 34

6 . CR Belouizdad [ Algeria ] = 27

7 . Simba SC [ Tanzania] = 24

8 . Petro de Luanda [ Angola ] = 24

9 . Pyramids [ Misri ] = 24

10 . Zamalek [ Misri ] = 23

11 . JS Kabylie [ Algeria ] = 22

12 . RS Berkane [ Morocco ] = 22

13 . USM Alger [ Algeria ] = 21

14 . Horoya [ Guinea ] = 18

15 . TP Mazembe [ DR Congo ] = 18

16 . Young Africans [ Tanzania ] = 16

17 . Orlando Pirates [ Afrika Kusini ] =16

18 . ASEC Mimosas [ Ivory Coast ] = 15

19 . Al-Hilal [ Sudani ] = 15

20 . ES Sètif [ Algeria ] = 14

NB : Viwango hivi vitaweza kubadilika baada ya Mashindano ya vilabu Afrika kuanza rasmi .



Alama [ Points ] za Timu Klabu bingwa [ CAF CHAMPIONS LEAGUE ] : 

Bingwa = 6

Mshindi wa pili = 5

Nusu fainali = 4

Robo fainali = 3

Nafasi ya 3 hatua ya makundi = 2

Nafasi ya 4 hatua ya makundi = 1 .



Alama [ Points ] za Timu Kombe La Shirikisho [ CAF CONFEDERATION CUP ] .

Bingwa = 5

Mshindi wa pili = 4

Nusu fainali = 3

Robo fainali = 2

Nafasi ya 3 hatua ya makundi = 1

Nafasi ya 4 hatua ya makundi = 0.5 



Alama zinavyogawanywa : 

2023 - 2024 = Alama za timu ×5

2022 - 2023 = Alama za timu × 4

2021 - 2022 = Alama za timu × 3

2020 - 2021 = Alama za timu × 2

2019 - 2020 = Alama za timu × 1



Alama 24 za Simba : 

2019 - 2020 : 0 × 1 = 0

2020 - 2021 : 3 × 2 = 6

2021 - 2022 : 2 × 3 = 6

2022 - 2023 : 3 × 4 = 12

2023 - 2024 : 0 × 5 = 0

Jumla Ya Alama : 0+6+6+12 = 24



Alama 16 za Yanga 

2019 - 2020 : 0 × 1 = 0

2020 - 2021 : 0 × 2 = 0

2021 - 2022 : 0 × 3 = 0 

2022 - 2023 : 4 × 4 = 16

2023 - 2024 : 0 × 5 = 0 

Jumla ya Alama : 0+0+0+16+0 = 16

Alama hizi hukusanywa kwa kipindi cha miaka mitano [ 5 ] na mfumo huu ulianzishwa rasmi na CAF mwaka 2017.


Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form