Wapenzi Wahalifu Waliotabiri Kifo Chao

 

6
Clyde Akiwa Amembeba Mpenzi Wake Bibiye Bonnie 
Hivi ulishawahi kufikiria kuwa na mpenzi ambaye mtaendana kwa tabia , kufanya kazi moja na kufa siku moja . Wahenga wanasema wa kufa na kuzikana .

Ngoja nikupeleke Marekani miaka ya 1930s kipindi cha Anguko kubwa la Uchumi ( Great Economic Depression ) ambapo tutawashuhudia hawa wapenzi wa kufa na kuzikana .

Clyde Champion Barrow alizaliwa mnamo 24 . 03 . 1909 kutoka kwenye familia ya kimasikini huko Texas . Ambapo alikuwa ni mtoto wa 5 kati ya 7 wa mzee Henry Barrow na Mwanamama Cumie Walker . Miaka ya 1920 familia yao ilihamia Mjini West Dallas ambapo ilikuwa ni sera ya kipindi hicho kuhamisha watu kutoka vijijini kwenda Mijini , familia yao iliishi kwenye Wagon ( Usafiri wa kutumja farasi kufungwa kwenye chombo ) kwa miezi kadhaa mpaka walipopata hela ya kununua hema na kuanza kuishi humo .

Clyde Barrow 
Kutokana na malezi yake ya umasikini kijana Clyde alijikuta akikamatwa na polisi kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 17 kwa kosa la kutorudisha gari alilokodi kwa wakati na kuwakimbia polisi .Pia mara ya pili alikamatwa yeye na kaka yake aitwaye BUCK kwa kosa la kuiba BATA MZINGA . 

Baada ya kumjua kwa ufupi kijana Clyde , ngoja tuhamie kwa bibiye Bonnie ...

Bonnie Elizabeth Parker alizaliwa mnamo 01 . 10 . 1910 huko Vijijini Rowena , Texas ambapo alikuwa ni mtoto wa 2 kati ya 3 wa Mzee Charles Parker na Emma Parker . Baba yake Bonnie alifariki 1914 kipindi hicho Bonnie Ana miaka 4 tuu . Mama yao Mjane akaamua kurudi na familia yake kwa wazazi wake huko West Dallas kutokana na ugumu wa maisha uliokuwa unawakabili . Mama yake aliamua kuwa mshonaji ili kukidhi mahitaji ya familia hiyo iliyokuwa haina Baba .

Bonnie Parker 
Akiwa High school Bonnie aliangukia kwenye Penzi na kijana aitwaye Roy Thornton na wakaamua kuacha shule na wakaona mnamo 15 . 09 . 1926 kipindi hicho Bonnie Ana miaka 15 na siku 358 na Roy Ana miaka 18 lakini ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu kutokana na Roy kwenda jela na hawakuonana tena kutoka mwaka 1929 mpaka kifo kinawakuta .

Lengo la stori hii sio penzi la Bonnie na Roy bali ni Bonnie na Clyde , sasa tuendelee ......

Kukutana Kwa Wapenzi Hao Waliotikisa Marekani.

Bonnie na Clyde walikuta mnamo mwaka 1930 kwa rafiki yao mmoja na hapo ndipo wakaanza kujuana , kipindi hicho Bonnie alikuwa na miaka 19 na Clyde miaka 20 . Baada ya penzi lao kushamiri na kupamba moto , Mambo yanageuka pale Clyde anapokamatwa na kwenda jela kwa kosa la kuiba gari hali iliyofanya Bonnie ajisikie vibaya sana kwa kuwa walishapendana mno na hakutaka mpenzi wake huyo aende jela na kumpoteza kama ilivyotokea kwa mpenzi na mume wake Roy aliyefungwa jela kwa miaka 5 . Waswahili wanasema Mapenzi Uchizi na ndiyo aliyofanya Bonnie . Baada ya kuona mpenzi wake yupo jela akaamua kwenda kumpenyezea bastola kimagendo siku ya kwenda kumtembelea gerezani .

Mnamo 11 . 03 . 1930 Clyde alitoroka gerezani pamoja na baadhi ya wafungwa wenzake kwa kutumia silaha aliyopewa na mpenzi wake kimagendo . Lakini bahati haikuwa kwao kwani wiki moja baadae walikamatwa tena na Clyde akahukumiwa miaka 14 gerezani na kufanya kazi ngumu huko Eastham State Farm . 

Akiwa gerezani bwana Clyde alikata kidole gumba na sehemu ya kidole kingine ili asifanye kazi ngumu sana akiwa gerezani.

Mama Anamtoa Gerezani Clyde

Unaweza kusema Clyde ni mwenye bahati sana au pia unaweza sema Uchungu wa mwana aujuaye mzazi , kwani mnamo mwezi wa 2 mwaka 1932 ambapo Clyde aliachiwa huru kutokana na Mama yake kuweza kumshawishi Hakimu na hivyo akapata fursa ya kuungana tena na mpenzi wake uraiani . Bonnie na Clyde wanaungana tena .

Na hapo ndipo safari yao ya mapenzi ikaongezewa na uhalifu ndani yake . Miezi miwili baada ya Clyde kutoka jela yaani mwezi wa 4 naye Bonnie akajiunga na kikundi cha uhalifu .Kuna msemo unasema " mwanzo mgumu " na ndivyo ilivyotokea kwa Bonnie kwani alikamatwa kwenye uhalifu ambao hawakufanikiwa kuutekeleza na kipindi akisubiri hukumu mahabusu , Bonnie alitumia muda wake mwingi kuandika mashairi , shairi Lake maarufu lilikuwa linaitwa " THE TRIAL'S END " ambapo mistari ya mwishoni ilisomeka 

 "Some day they'll go down together / And they'll bury them side by side / To few it'll be grief / to the law a relief / but it's death for Bonnie and Clyde."

Hili shairi linasemekana kuwa Bonnie alijitabiria kifo chake pamoja yeye na mpenzi wake Clyde ambalo kwa kiswahili lilisomeka " siku moja wataenda chini pamoja na watazikwa pamoja , kwa wachache itakuwa majonzi , kwa vyombo vya sheria itakuwa nafuu lakini hicho ni kifo cha Bonnie na Clyde " Hili shairi aliliandika mwaka 1932 na kujitabiria kifo Chao. Baadae Bonnie aliachiwa huru baada ya kujitetea kuwa hakuhusika na kikundi hicho na yeye alikuwa mateka wa kikundi hicho . Baada ya kuachiwa akaungana na mpenzi wake Clyde ambapo yeye hakuweza kukamatwa kwenye tukio hilo .

Jumba Ambalo Kundi Hilo Lilikuwa Linajificha Na Kupanga Uhalifu Wao 
Hivyo wawili hao wakaungana na kijana Raymond Hamilton ambaye ni mtaalamu wa bastola . Kukundi kikawa na watu watatu baadae Mwezi wa 11 1932 Hamilton alikamatwa na kuhukumiwa zaidi ya miaka 200 jela kutokana na makosa yake , kwenye kikundi hicho na nafasi yake ikachukuliwa na Wiliam Jones na kuendelea na uhalifu wao .

Mnamo 23 .03 .1933 Ivan Barrow ( kaka yake na Clyde ) anaachiwa kutoka gerezani na baada ya kutoka gerezani anaungana na mdogo wake uraiani kwenye kukundi cha uhalifu . Ivan anakuja na mkewe aitwaye Blanche , hivyo kikundi kinakuwa na watu wa 5 yaani ( Bonnie, Clyde , William, Ivan na Blanche ) . Kikundi hicho kikaendeleza uhalifu wa wizi maeneo mbalimbali na kuepuka kukamatwa mara kadhaa . 

Baada ya kuwa wahalifu sugu Polisi wakaanza kuwasaka kwa nguvu kubwa hali iliyopelekea Ivan Barrow kujeruhiwa vibaya na mke wake Blanche kukamatwa mnamo 29 . 07 .1933 . William naye alikamatwa November 1933 huko Huston , Texas kwenye tukio la uhalifu ambao Bonnie na Clyde walifanikiwa kutoroka hivyo kufanya kundi hilo linaloitwa BARROW kubaki na watu wa 2 na ni mtu na moenzi wake .

Msako ukaendelea na BARROW GANG ilitambulika kila kona na walisakwa kwa nguvu kubwa mno , hatimaye mnamo 22 . 11 . 1933 Polisi wa Dallas, Texas wakaweka mtego ili kuwakamata wapenzi hao lakini walifanikiwa kutoroka kwa mara nyingine tena na katika kuwakimbia Polisi walimteka Wakili na kuchukua gari yake kisha kuitelekeza huko Miami , Oklahoma na wakawapotea tena Polisi . 

Askari Pamoja Na Maafisa Waliokuwa Wanawafuatilia Bonnie Na Clyde 
Waswahili wanasema mazoea hujenga tabia na ndivyo ilivyokuwa kwa wapenzi hao kwani mnamo 21 . 12 . 1933 walifanya uhalifu mwingine wa kupora watu na kuiba Mali zao huko Shrevport , Louisiana . 

Mnamo 16 . 01 . 1934 Bonnie na Clyde walifanikiwa kuwatorosha wafungwa watano waliokuwa wanasafirishwa na mmoja wa wafungwa hao alikuwa mhalifu mwenzao kwenye kundi la BARROW aitwaye Raymond Hamilton. Katika shambulio hilo polisi wawili walipigwa risasi na wafungwa hao .

Wapenzi hao waliendelea na matukio yao hali iliyofanya msako uzidi kuwa mkali hasa pale walipomteka na kumjeruhi Polisi Chief huko Miami , Oklahoma walipokimbilia tukio lilitokea 06 . 04 . 1934 na pia siku tano nyuma yaani 01 . 04 . 1934 waliwapiga risasi walinzi wawili waliokuwa wanafanya patrol maeneo hayo .

Kutokana na kukithiri kwa matukio ya wapenzi hao wawili , FBI nao wakaingilia kati kesi hiyo na kufanya hali izidi kuwa ngumu kwa Bonnie na Clyde. Picha zao na taarifa muhimu zilibandikwa maeneo mbalimbali na pia kila Afisa wa FBI alipewa taarifa hizo ili kuwakamata wapenzi hao .

Bonnie Na Clyde Walichapishwa Kwenye Gazeti Wakitafutwa Kwa Uhalifu Wao 
Mafisa wa FBI wakaanza kufuatilia hatua zote walizokuwa wanapita na kutega maeneo hayo ili kuwasubiri wajitokeze kwani muda huo ilisemekana wapenzi hao walikuwa wamejificha huko vijijini Lousiana .

Kwenye kufanya upelelezi maafisa wa FBI wakagundua kuwa Bonnie na Clyde walikuwa wanafanya sherehe huko Black Lake , Lousiana mnamo 21 . 05 . 1934 na walipata taarifa kuwa watarejea baada ya siku mbili .

Kila Chenye mwanzo kina mwisho na mnamo 23 . 05 . 1934 Bonnie na Clyde walikuwa wanarejea kutoka kwenye sherehe na bila ya kutambua lolote kuwa wanasubiriwa na maafisa wa FBI pamoja na polisi kutoka Texas na wa hapo Lousiana. Baada ya kutokea na gari yao mchana huo wakiwa wamezungukwa ikavbidi watake kuanza kukimbia na gari yao lakini waliishia kupigwa risasi na kufariki papo hapo wote wakiwa pamoja kama alivyotabiri bibiye Bonnie. 

Jinsi gari yao ilivyomiminiwa risasi na askari hao waliokuwa wakiwasubiri 

Miili ya Bonnie Na Clyde Baada ya kushambuliwa na maafisa wa polisi na kupelekea kufariki papo hapo ndani ya gari yao 
Na huo ndiyo ukawa mwisho wa maisha ya wapenzi hao lakini jina lao bado linaishi hadi leo kwenye uso wa dunia .


Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form