AVATAR : THE WAY OF WATER YAINGIA SITA BORA

 


Filamu ya AVATAR THE WAY OF WATER ambayo ni muendelezo wa Filamu ya AVATAR ( 2009 ) kwa sasa imefikisha zaidi ya Shilingi Trilioni 4.68 ( USD 2.02B ) kwenye mapato yake toka ilipoachiwa mnamo tarehe 16 . 12 . 2022 .

Filamu hiyo inakua filamu ya Sita ya muda wote duniani inayoingiza mapato mengi na pia  kufikisha kiasi cha zaidi ya Shilingi Trilioni 4.68 ( USD 2B ) kwenye mapato yake ( boxoffice ) . Filamu nyingine zilizofikia kiasi hicho ni 

1 . AVATAR ( 2009 ) : Shilingi Trilioni 6.83 ( USD 2.92B ) 

2 . AVENGERS:ENDGAME ( 2019 ) : Shilingi Trilioni 6.54 ( USD 2.79B )

3 . TITANIC ( 1997 ) : Shilingi Trilioni 5.12 ( USD 2.19B ) 

4 . STAR WARS : THE FORCE AWAKENS ( 2015 ) : Shilingi Trilioni 4.84 ( USD 2.07B ) 

5 . AVENGERS : INFINITY WAR ( 2018 ) : Shilingi Trilioni 4.79 ( USD 2.05B ) 


Pia Mwandishi , Mtengenezaji na Muongozaji wa filamu anayejulikana kama  JAMES CAMERON anakuwa ni Mtengenezaji wa filamu wa kwanza kutengeneza filamu zilizofikisha zaidi ya Shilingi Trilioni 4.68 ( USD 2B ) ambazo ni AVATAR (2009) , TITANIC (1997) na AVATAR : THE WAY OF WATER (2022) . ( 🖊 Luqman Kisokora ) 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form