Teknolojia Ilipelekea Avatar Kutoachiwa Mwaka 1999

 


Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa filamu au hata kama sio mfuatiliaji mzuri  lazima utakuwa ushaona au kusikia habari za filamu ya AVATAR  yenye mchango mkubwa sana kwenye mabadiliko ya teknolojia  upande wa Utengenezaji filamu .

Filamu hiyo ambayo ilitoka rasmi tarehe 18 . 12 . 2009 na  ndiyo inayoongoza kwa kuingiza mapato mengi duniani kwa muda wote ikiwa imeingiza takribani Shilingi za kitanzania Trilioni  6.83 ( USD 2.923B ) Ina historia kubwa nyuma yake kabla ya kuachiwa mnamo karne ya 21 .

Historia ya filamu hiyo inarudi nyuma karne ya 20 mnamo mwaka 1994 ambapo mzalishaji na mwandishi wa filamu James Cameron alipoanza rasmi uandishi wa filamu hii na kuandika kurasa 80 tuu . Alihamasishwa uandishi wa filamu hii kutokana na vitabu mbalimbali alivyovisoma toka akiwa Mtoto .

Mwaka 1996 James Cameron Alitangaza kuanza kuzalisha filamu ya AVATAR baada ya kumaliza filamu ya TITANIC . 

Lengo lilikuwa ni kuanza kuzalisha katikati ya Mwaka 1997 na ifikapo mwaka 1999 filamu hiyo iachiwe rasmi  Lakini James Cameron Aliamua kukatisha uzalishaji wa filamu hiyo kutokana na kuona kuwa kwa Miaka hiyo teknolojia ilikuwa ya chini na haitoshi kuzalisha filamu hiyo ambayo ilikuwa inahusu miaka ya 2154 karne ya 22 .

James Cameron alisubiri kwa miaka kadhaa na hatimaye mwaka 2009 alikuja kutuletea moja ya filamu bora kabisa kuwahi kuzalishwa kwenye historia ya filamu 

( 🖊 Luqman Kisokora )


Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form