UKISAFIRI LEO UTAFIKA JANA!


 Je Wajua?

Wakati unapanga safari kutoka Tokyo Japan kuelekea Honolulu amboa ndio mji mkuu wa jimbo la Hawaii katika United State(U.S) inakupasa utambue kuwa miji hiyo iko katika maeneo tofauti ya majira,na Honolulu iko nyuma ya Tokyo kwa masaa 19.Hivyo basi kama Tokyo ni Jumanne saa 1 asubuhi basi Honolulu itakuwa ni Jumatatu saa 6 mchana.Na kwa kawaida safari ya ndege baina ya Tokyo na Honolulu ni masaa 7,hivyo ikiwa utatoka Tokyo kuelekea Honolulu jua kabisa utakuwa unarudi nyuma kimasaa,Kwa mfano ikiwa utatoka Tokyo hiyo Jumanne ya saa 1 asubuhi basi utawasili katika mji wa Honolulu siku ya Jumatatu saa 1 jioni. (🖋️Hashim Seki)



Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form