Vin Diesel Kulipwa Takribani Shilingi Bilioni 47 Za Kitanzania Kwa Fast X


Muigizaji mashuhuri na maarufu kwenye mfululizo wa filamu za FAST AND FURIOUS aitwaye VIN DIESEL ameripotiwa kulipwa takribani Shilingi Bilioni 46.7 za kitanzania (USD 20M) kwenye uhusika wake kwenye filamu ya FAST X ( FAST AND FURIOUS 10 ) .

Filamu hiyo imeshesheni waigizaji wengine mashuhuri kama vile Jason Statham, Michelle Rodriguez, Jason Momoa, John Cena, Brie Larson, Tyrese Gibson, Chris "Ludacris" Bridges, Jordana Brewster, Nathalie Emmanuel, Sung Kang, Scott Eastwood, Michael Rooker, Daniela Melchior, Alan Ritchson, Helen Mirren, Cardi B, Rita Moreno, and Charlize Theron. Huku pia kukiwa na tetesi kuwa GAL GADOT( maarufu WONDER WOMAN ) anaweza kurudi tena kwenye filamu hiyo .

Bajeti ya filamu hiyo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 793.9 za kitanzania (USD 340M) huku takribani Shilingi Bilioni 233.5 za kitanzania (USD 100M) zimetumika kuwalipa waigizaji hao .

Filamu hiyo inatarajiwa kutoka mnamo tarehe 19 . 05 . 2023 ( 🖊 Luqman Kisokora ) 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form