Ardhi Ya Urusi Iliyouzwa Marekani Senti 2 Kwa Heka Moja

Marekani na Urusi ni nchi zenye upinzani mkubwa hasa kwenye swala la Uchumi . Je ushawahi kujiuliza ilikuwaje mpaka Urusi ikaamua kuuza ardhi yake kwa Marekani?. Kuna msemo unasema " Hakuna Mpinzani wa  kudumu " . Sasa twende moja kwa moja kujua kilichojiri kwenye biashara hiyo iliyotokea karne ya 19 .

Jimbo la Alaska linapatikana  Bara la Amerika kaskazini mwa nchi ya Canada . Jimbo hilo ni moja ya majimbo yanayounda taifa la  Marekani na lina historia ya kuwa chini ya utawala wa Urusi kabla ya karne ya 19 Mwishoni .Alaska iligunduliwa na Mpelelezi aliyeajiriwa na Urusi aitwaye Vitus Boring mnamo mwaka 1741 na aliutaarifu Utawala wa Urusi juu ya ardhi hiyo .
Na ilipofika mwaka 1784 Wafanyabiashara kutoka Urusi waliweka makazi yao hapo na Ukawa mwanzo wa makazi ya Urusi huko Alaska , Amerika . Na Jimbo hilo likiwa chini ya Utawala wa Urusi mpaka Mwaka 1867 .

KUUZWA KWA ALASKA .
Kutokana na Vita ya Creamean baina ya Urusi dhidi ya [ Ottoman , Uingereza na Ufaransa] Urusi walishindwa Vita hiyo dhidi ya Ulaya na kupelekea kudhoofika Kiuchumi na kushindwa kushikilia baadhi ya Makoloni yake . 
Moja ya Makoloni hayo ni Alaska ambapo ilikuwa mbali na Urusi , pia Urusi ilihofia mashambulizi mengine kutoka kwa Uingereza ambayo ilikuwa inatawala Canada .
Hivyo Urusi waliamua kuiuza ardhi ya Alaska kwa Marekani ambayo ilikuwa inatanua himaya yake zaidi Magharibi ili wapate fedha zaidi .
Mnamo tarehe 30 . 03 . 1867 , Urusi waliiuza himaya ya Alaska kwa USD 7.2M . Ambayo ni sawa na chini ya Senti 2 kwa Heka moja . Na Marekani walipata zaidi ya 600, 000 square miles ( Ukubwa wa Takribani Mara 2 ya Mji wa Texas ).
Hundi ya USD 7.2 Million 

Baadhi ya Wapinzani wa Serikali ya Marekani kipindi hicho waliponda sana mkataba huo kwa k7usema kuwa ardhi hiyo ni mbaya na imekaa porini na haina Mali yeyote .

UCHUMI WA ALASKA ULIVYOSTAWI ZAIDI 
Mambo yalibadilika pale mwaka 1899 ambapo DHAHABU iligundulika huko Alaska na biashara zilizidi kukua mno .
Kwasasa 25% ya Mafuta ya Marekani yanatokea huko na zaidi ya 50% ya Chakula cha baharini nchini Marekani kinatokea huko .
Mji wa ALASKA unatokana na neno Alyeska ambapo maana yake ni " GREAT LAND " . yaani ardhi yenye thamani kubwa .

Mji huo unatambuliwa sana kwa uwepo wa AURORA BOREALIS yaani Anga yake huwa inawaka muda wa usiku na kuwa na muonekano angavu wenye rangi mbalimbali za kuvutia .


Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form