Bajau ni jamii ya watu wanaopatikana kwenye Bara la Asia maeneo ya Ufilipino , Malaysia , Indonesia na Bruinei . Idadi yao inakadiriwa kuwa Takribani Milioni 1.2 duniani kote .
Sifa kubwa ya Wabajau ni kuishi maeneo ya baharini wakiwa na Nyumba zilizotengenezwa mfano wa Boti ili ziwaweshe kuhama sehemu moja kwenda nyingine ndiyo maana huitwa " SEA NOMADS " na hutumia takribani 60% ya Siku yao wakiwa ndani ya Maji . Huku wakiwa na uwezo wa kuzama kwa dakikia 13 kwenye kina cha Mita 70 . Hali hii siyo ya kawaida kwa binadamu , kwani Binadamu wa kawaida tunatumia Sekunde kadhaa kuzama ndani ya maji au dakika kadhaa kwa wale wenye mazoezi na uzoefu .
Pia Wabajau wana uwezo wa kuona vizuri ndani ya maji kuliko watu wengine na kupelekea kukusanya vyakula chini ya bahari na kuvua samaki wakiwa ndani ya maji bila ya msaada wowote wa vifaa vya macho .
Baada ya Utafiti zilizofanywa imekuja kugundulika kuwa Watu wa jamii ya Bajua wana BANDAMA ( SPLEEN ) yenye ukubwa wa 50% zaidi ya watu wa kawaida , hivyo kunawafanya watu wa Jamii hiyo kufanya wawe na akiba kubwa ya damu yenye hewa ya Oksijeni kwenye bandama zao , hivyo kupelekea kuweza kubana pumzi kwa muda mrefu wanapokuwa ndani ya Maji bila ya shida yeyote kwani hewa ya oksijeni inakuwa imetunzwa kwa wingi kwenye Bandama zao .
Pia Ndani ya Seli zao zimeonekana kuwa wana vinasaba vya utofauti na watu wengine ambavyo vinapelekea waweze kukaa sehemu zenye kiwango kidogo cha Oksijeni na kuweza kuogelea chini ya kina kirefu ( Zaidi ya Mita 70 )bila ya vifaa vyovyote vya kuogelea na kutopata athari zozote .
Maisha ya jamii ya Bajau siku zote ni kuzaliwa , kuishi na kufariki wakiwa baharini , Mara nyingi huenda nchi kavu kuuza samaki na bidhaa nyingine za baharini ili waweze kupata mahitaji yao mengine muhimu
Source : (Baranova et al., 2017).
Tags
Stories