Daktari Kane Akiwa Anajifanyia Upasuaji |
Basi turudi nyuma huko Marekani tukamshuhudie huyo Mganga aliyejiganga . Hakujiganga kwa kubahatisha kwa sababu alifanya hivyo zaidi ya mara moja na anafahamika kama Daktari Evan Kane .
Dr Evan O'Neil Kane alizaliwa mnamo tarehe 06 . 04 . 1861 huko Pennysylvia Marekani kwenye familia ya Jenerali Thomas Kane na Tabibu Elizabeth Wood Kane .
Evan alikuwa mtoto wa 3 kati ya watoto wa 4 wa familia ya Mzee Thomas Kane .
Kwenye watoto hao wanne , watatu walikuja kuwa Matabibu kama ilivyokuwa kwa Mama yao ambao ni Harriet , William na Evan huku ndugu yao mmoja ambaye ni Elisha alikuja kuwa Mhandisi .
Kwa kifupi familia ya Evan ilikuwa ni familia ya kisomi na watu wenye hadhi .
Kane alimaliza masomo yake huko Philadelphia kwenye chuo cha JEFFERSON MEDICAL mnamo mwaka 1884 na Akaja kufanya kazi kwenye Hospitali ya KANE SUMMIT iliyoanzisha na Mama yake aitwaye ELIZABETH KANE kwa kumuenzi Mume wake Jenerali kane ambaye aliamini eneo hilo lina hewa nzuri na vidonda vinapona vizuri , baadae Dr Kane kuwa Daktari Mkuu Wa Upasuaji katika hospitali hiyo .
Daktari Evan O'Neil Kane |
Dr Kane anatambuliwa zaidi kwa kujifanyia upasuaji yeye mwenyewe na Alikuwa anaamini baadhi ya Upasuaji unahitaji Local Anasthesia ( ganzi ya kiungo husika ) na sio general Anaesthetia ( ganzi ya mwili mzima ) .
Hivyo aliamua kujifanyia mwenyewe upasuaji ili ajionee maumivu wanayoyapata Wagonjwa na kujua kama wataweza kuvumilia au laa .
UPASUAJI WA KWANZA
Mnamo mwaka 1919 akiwa na miaka 58 , Daktari huyo alijifanyia upasuaji wa kuondoa kIdole chake kimoja kilichikuwa na maambukizi .Na upasuaji huo ulienda vizuri kabisa
UPASUAJI WA PILI
Huu ndio upasuaji wake uliompa zaidi umaarufu na kutambulika zaidi ambapo Aliondoa Kidole tumbo ( Appendix ) chake akiwa kwenye Local Anasthesia ( ganzi ya kiungo husika kinachofanyiwa upasuaji ) . Hii ilikuwa ni mnamo tarehe 15 . 02 .1921 akiwa na Umri wa miaka 60 . Akiwa amezungukwa na vioo .
UPASUAJI WA TATU
Waswahili wanasema Jasiri haachi asili , Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Dr Kane .
Kwani mnamo mwaka 1932 akiwa na umri wa miaka 70 alijifanyia upasuaji wa kurekebisha ngiri ( Inguinal hernia ) ambapo aliipata baada ya ajali ya kuendesha farasi miaka 6 nyuma .
Upasuaji huu ulihudhuriwa na Waandishi wa habari mbalimbali na ulifanyika kwenye hospitali ya KANE SUMMIT .
Upasuaji huu ulikuwa ni wa hatari zaidi ya zile pasuaji za mwanzo kutonana na kuwepo kwa uwezekano wa kupasua mshipa wa damu ( femoral artery ) . Na ilichukua takribani Lisaa 1 na dakika 45 kwa upasuaji huo kukamilika . Inaelezwa kuwa akiwa anajifanyia upasuaji huo Dr Kane alikuwa akipiga stori na kutaniana na Wauguzi .
Kwa kawaida baada ya upasuaji huo inatakiwa wiki 6 za kupumzika lakini Dr Kane chini ya siku 2 alirudi tena hospitali na kuendelea na kufanyia Upasuaji Wagonjwa wengine akishirikiana na Dr Cleveland.
KAZI NA MUZIKI
Dr Kane alikuwa una utaratibu wa kusikiliza muziki kwa kutumia Santuri ( Phonograph ) akiwa anawafanyia Wagonjwa wake Upasuaji. Aliamini hii ilikuwa na njia nzuri ya kutengeneza utulivu na kufanya akili ifanye kazi kwa umakini zaidi . Pia ilisaidia Wagonjwa wake wawe na utulivu mkubwa wakiwa wanasikiliza mziki laini , kwani aliamini kuongea na mgonjwa kipindi cha upasuaji kunapunguza umakini wa Daktari , lakini muziki ilikuwa ni njia bora .
Baadae research zilikuja kudhibitisha kuwa muziki ni mojawapo ya njia nzuri ya kuounguza maumivu na kufanya mtu ajisikie vizuri.
Mfano wa Santuri aliyokuwa akitumia Dr Kane kusikiliza muziki anapofanya upasuaji |
UPASUAJI RELINI .
Mwishoni mwa karne ya 19 huko Amerika Miji mingi ilikuwa inajengwa na njia kuu ya Usafirishaji ilikuwa ni Reli . Hivyo nguvu kazi ilikuwa ni kubwa kwenye kutengeneza Reli nchi nzima kwa ujumla .
Kutokana na watu wengi na pia ajali zilikuwa zinatikea kwa kiwango kikubwa mno .
Hivyo Dr Kane aliwahi kufanya kazi kama Daktari wa Upasuaji Relini akihusika na ajali zinazotokea kupindi cha ujenzi .
Inaelezwa kwa kipindi cha miaka 3 yaani 1898 - 1900 , Dr Kane alifanya Upasuaji kwa zaidi ya Watu 1,000 kutoka na ajali zinazotokea kwenye shighuli za relini.
MWANAYE KWENYE KESI YA MAUAJI.
Mtoto wa Dr Kane aitwaye Elisha Kane ambaye ni mkuu wa idara moja kwenye chuo cha TENNESSES alishutumiwa kwa mauaji ya Mkewe( JENNY KANE ) kwa kumzamisha kwenye fukwe ya CHESAPEAKE BAY .
Kesi hiyo iliibua hisia za watu mbalimbali na siku ya kusikilizwa kwa hukumu hiyo watu wengi walijaa Mahakamani mpaka wengine walikosa nafasi na kukaa nje. Dr Kane alikuja kutoa taarifa za uchunguzi wa marehemu na kuonekana kuwa Jenny alikuwa na tatizo la moyo ambalo lilipelekea kuzama kwenye maji baada ya tatizo hilo kumshambulia ghafla . Hivyo mtoto wa Dr Kane alikuwa hana hatia na mashitaka juu ya kumuua mkewe yalifutwa .
KUFARIKI
Daktari Evan Kane alifariki mnamo tarehe 01 . 04 . 1932 akiwa na umri wa miaka 71 kutokana na kusumbuliwa na Pneumonia. Huku akiacha mke na watoto 7 .