Ona video ya simulizi yote kwa kiswahili 👇 (au Soma)
Binti huyu alikuwa amebarikiwa kipaji na uwezo mkubwa wa kiakili licha ya kuzaliwa kwenye familia ya kimasikini mno na bado alikuwa na lengo la kujiendeleza kimasomo zaidi, lakini angewezaje sasa na jamii ya miaka hiyo haikuruhusu mtoto wa kike kusoma?
Basi hali ya maisha ilivyozidi kuwa ngumu Margaret na mama yake wakahamia London kwa Mjomba wake na Margaret aitwaye James Barry ambaye alikuwa ni msomi na mchoraji mwenye fedha za kutosha.
Kufa Kufaana
Mnamo Mwaka 1806 Margaret alipata pigo kubwa baada ya mjomba wake huyo aliyekuwa mkombozi wake na mtu aliyekuwa akiwapatia mahitaji muhimu kufariki Dunia.Hivyo kumuacha yeye na mama yake kwenye huzuni na maumivu makubwa
Lakini waswahili wanasema "kufa kufaana" Yaani kifo cha Mjomba wake James Barry kilifungua ukurasa mpya kwenye maisha ya Margaret,
Je ni ukarasa gani huo ulifunguka kwenye maisha ya Margaret?
Kufuatia kifo cha Mr James Barry,ndipo Margaret akaona hiyo ndiyo fursa ya yeye kuendeleza ndoto yake ya muda mrefu aliyokuwanayo
Hivyo Margaret akachukua na kuanza kutumia jina la mjomba wake na kuanza mwanzo mpya wa safari yake ya kimasomo kama mwanaume,yaani sasa Margaret ni Mr James Barry.
Margaret Ajiunga Na Chuo Cha Utabibu
Mnamo Mwaka 1809 Margaret ambaye sasa ni James Barry alijiunga na Chuo cha Utabibu cha Edenburg na watu wengi pale chuoni walikuwa na mashaka juu ya muonekano wake na wengi walimuona kama ni mtoto mdogo kutokana na kuwa na ngozi laini mno, kimo kifupi na sauti isiyo nzito,Kumbe hawakujua kuwa huyo alikuwa ni mwanamke aliye kwenye muonekano wa kiume.
Watu wengi kipindi hicho hawakushtuka au kuwa na mashaka zaidi kwa kuwa walijua mwanamke asingeweza kusoma elimu yeyote kutokana na kutoruhusiwakwao.
Margeret kutokana na uwezo wake mkubwa wa kiakili alipohitimu masomo yake ya utabibu alijiunga na jeshi la uingereza Mwaka 1813, Alizunguka Maeneo mbalimbali ya Dunia kama vile Afrika kusini na kufanya kazi kama Daktari msaidizi chini ya jeshi la uingereza .
Apangiwa Kazi Afrika Kusini
Baadaye akapandishwa cheo na kuwa Assistant Staff Surgeon Liutenant na akahamia cape town South Africa akafanya kazi kwa miaka 10
Akiwa huko,Margaret alikuwa na urafiki wa karibu na Gavana Lord Charles Somerset na kutokana na ukaribu wao kuna baadhi ya watu wanahisi kuwa Gavana Lord Charles aliijua Siri ya Margaret ya kuwa hakuwa mwanaume na walikuwa ni wapenzi wa siri. Lakini watu wengi walijua kuwa walikuwa ni wapenzi wa jinsia moja kwakuwa hawakujua kuwa James Barry ambaye ni Margaret ni Mwanamke na sio mwanaume
Dr James Barry ambaye ni Margaret anatambulika kwa kufanya mambo makubwa kwenye kazi yake kama vile;
Alikuwa ni mtu wa kwanza kufanya upasuaji wa mama na mtoto na kufanikiwa kwa asilimia 100 ndani ya Afrika Kusini.
Alitibu masikini,watumwa na watu mbalimbali.
Pia anakumbukwa kwa Kuhamasisha usafi wa Mazingira ili kuepuka Magonjwa ya mlipuko,
Ilipofika mwaka 1857 alipandishwa cheo na kuwa inspector general sawa na Brigedia general.
Siri Yafichuka
Margeret Ann alifariki mnamo Tarehe 20/07/1865 akiwa hoi kitandani kwa dysentery baada ya kuugua kwa muda mrefu kitandani.
Je Siri yake ya kuwa yeye ni mwanamke na sio mwanaume iligundulika vipi?
-Katika siku za mwisho za uhai wake akiwa hoi kitandani alitoa ombi la kutaka kuzikwa akiwa na nguo zake. Lakini baada ya kufariki ombi lake halikutekelezwa kutokana na hadhi yake,Hivyo nesi aliyekuwa akumuosha na kumuandaa aligundua vitu vikubwa viwili na vya kushangaza ambavyo ni ;
1 .Jinsia ya kike
2 .Alama kwenye tumbo lake zilizoonesha kuwa aliwahi Kupata ujauzito katika kipindi cha nyuma.
UJAUZITO huo ulikuaje?
Inasemekana kuwa kwenye kipindi cha usichana wake Margeret aliwahi kubakwa na Kupata mimba na kujifungua mtoto aitwaye Juliana ambaye alilelewa na mama yake Margaret, Bi Marry, hivyo watu wengi walikuwa wakijua kuwa Juliana ni mdogo wake na Margeret kumbe alikuwa ni mwanaye wa kumzaa.
Margaret au Dr James Barry alizikwa Kensal Green Cementry katika Northwest London na alipewa heshima ya kuwa mwanamke wa kwanza kwenye kizazi chake kuwa tabibu au daktari wa kwanza.
Mtafiti & Mwandishi: Luqman Zuberi Kisokora
Mhariri & Mwandaaji: Hashim Seki
Msimuliaji: Hassan Nasibu
Video :YouTube: 99 TZ