Filamu ya PATHAAN imeweka rekodi na kuwa filamu ya kwanza kwenye kiwanda cha filamu cha BOLLYWOOD kuingiza zaidi ya Shilingi Bilioni 180.78 za kitanzania ( USD 77M ) ndani ya wiki moja . Filamu hiyo imetoka mnamo 25 . 01 . 2023.
PATHAAN inakuwa filamu ya kwanza ya SHAH RUKH KHAN kufikisha mapato hayo na pia inakuwa filamu ya kwanza ya SRK toka mwaka 2018 ambapo alitoa filamu ya ZERO na amepumzika kwa takribani miala mitano ( 5 ) kwenye kuigiza filamu kama muhusika mkuu.
Ndani ya wiki moja tu Filamu imeingia kwenye orodha ya filamu zilizoingiza mapato mengi kwa upande wa BOLLYWOOD za muda wote na kushika nafasi ya 5.
Filamu hiyo inahusu Polisi mpelelezi ( SHAH RUKH KHAN ) anajifanya kama Mwizi na Muuza madawa ya kulevya ili kuweza kumkamata Mhalifu mmoja sugu ndani ya Mji mmoja huko Mashariki ya kati . Mji huo ni makazi ya Wahalifu wengi , vikundi vya kuhuni pamoja na biashara zote chafu kama vile Madawa vya kulevya.
Filamu hiyo inatarajiwa kupatikana kwenye tovuti za kutazama na kupakua filamu ( streaming services ) mnamo tarehe 25 . 04 . 2023.
Tags
Movies