Sio Salama Kutumia WhatsApp Mods; GB, FM, Fouds, Yo n.k


Watu wengi hasa wanaotumia simu za Android hupendelea sana kutumia WhatsApp Mods kwakuwa kuna mambo mengi ambayo WhatsApp ya kawaida (official WhatsApp) haifanyi.

kwenye WhatsApp ya kawaida kuna limit ya matumizi katika vitu mbalimbali, Lakini ukiwa na WhatsApp Mods kama vile GB WhatsApp , FM WhatsApp, Fouds, Yo, GoWhatsApp, WhatsApp plus, prime n.k  unaweza fanya mambo ambayo kwenye WhatsApp ya kawaida hakuna kama vile

>> Ku-share kwa mara moja kwa zaidi ya watu watano (mpaka watu 250)

>> kuweka status ndefu ya zaidi ya sekunde 30

>> Kuficha last seen

>> Kuficha status view

>> uwezo wa kusoma na kuona message au status zilizofutwa

>> kubadili muonekano wa whatsApp yako kuwa kwa namna nzuri unayoitaka

>>uwezo wa kuzuia view once (yaani mtu anatuma uone mara moja tu) n.k

WhatsApp Mods sio nzuri kutumia kama unajali taarifa zako binafsi kukuhusu wewe, asilimia kubwa za WhatsApp Mods ndani yake kuna kirusi (mobile trojan) ambacho kinashambulia simu yako na kudukua taarifa zako muhimu kuanzia kusoma sms, kinaweza kukuletea matangazo wakati wowote pia kuuza taarifa zako.

WhatsApp Mods sio end to end encryption maana yake message zako unazo tuma au kutumiwa basi mtu yeyote mwingine anaweza kuzipata kiurahisi na kuzisoma.

Pia unaweza kuwa banned wakati wowote (Yaani namba yako kufungiwa isiweze kutumia tena WhatsApp) kutoka Kwenye kampuni official ya WhatsApp maana hawapendi watu wawe wanatumia hizi programs.

Pia kama unatumia hizi mods za WhatsApp ambazo sio official ni ngumu kufanya backups za data zako (yaani kurudisha taarifa zako za awali) na ikitokea umefanya backup basi mara nyingi sio taarifa zote zinazorudi, Hivyo sio salama kutumia WhatsApp Mods. ( 🖋️ Hashim Seki )

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form