" Utanitumia picha zangu Telegram " , " Ingia Xender unitumie " . Hizi kauli wanazisikia sana watumiaji wa Tunda ( IPhone ) . Na ndo watu wanaongoza kwa kupiga sana picha na kufuta sana picha . Yaani akishakutumia picha zako kinachofuata ni kudelete tuu ila sio kwa ubaya .Leo sitaki kuwazungumzia Watumiaji wa Tunda ila nataka kuzimungumzia Tunda lenyewe .
Katika simu ambazo zinazisifiwa kwa kupiga picha kali basi ukiweka orodha yeyote lazima IPhone iwe ya kwanza . Watu wengi wananunua iphone kwa pride au uwezo wake mzuri wa kupiga picha ila kuwa wale kwasababu ya security na privacy yake ya juu .
Je unajua hiyo kamera kali unayoisifia ya Iphone anatengeneza nani ? Na yupo wapi ?. Sasa Turudi Nyuma kidogo ...
Iphone ya kwanza kabisa ilitengenezwa mwaka 2007 na baada ya mafanikio makubwa na umaarufu hasa kwenye camera zake . Kama kawaida wanasema "Ukiona vyaelea , ujue vimeundwa " watu wengi walianza kufatilia kujua mtengenezaji wa kamera hizo .
Iphone 4S |
Na hatimaye mnamo December 12 Mwaka 2022 . Mkurugenzi Mkuu wa Apple bwana Tim Cook alimtembelea Ken Yoshida , Mkurugenzi wa Sony huko Kumamoto , Japan na alitupia kwenye Twitter akisema " We’ve been partnering with Sony for over a decade to create the world’s leading camera sensors for iPhone " .Akimaanisha kuwa " Tumekuwa na Ubia ( ushirikiano ) na Sony kwa zaidi ya miaka 10 ya kutengeneza kamera bora kabisa duniani " .
Huo ndo ukawa mwanzo wa taarifa rasmi kutoka Apple kuwa kamera zao zinazalishwa na Mjapani . Mtaani kwetu wanasema "lisemwalo lipo " na zile tetesi za mwaka 2011 zimekuja kuthibitishwa na Iphone wenyewe .
Siku zote kitu bora ni muunganiko wa mawazo mbalimbali na ndiyo maana Iphone wameamua kushirikiana na kampuni mbalimbali zinazofanya vizuri duniani ili kupata kitu bora .