Mfahamu Simba Bob Junior Aliyekuwa Mfalme Wa Serengeti

Mfalme ameuawa , hii ni kauli maarufu mno kwa sasa nchini Tanzania hasa kwenye sekta ya utalii .
Mfalme huyu si mwingine bali ni BOB JUNIOR , Simba maarufu na mtawala wa serengeti yaani ndiye aliyekuwa mfalme wa Hifadhi ya Serengeti ,
Simba huyu ametawala serengeti kwa takribani miaka 7 huku akishirikiana na kaka yake aitwaye TRYGGVE . Na yeye anajulikana pia kwa jina la SYNGGVE ambaye anakadiriwa kuwa na miaka 10 .
Kaka yake Bob junior ( Tryggve ) naye inasemekana ameuawa na wapinzani wao siku za nyuma , hivyo Serengeti imepata wafalme wapya . Waswahili wanasema Wafalme hufa lakini Ufalme siku zote upo . Baada ya takribani miaka 7 ya utawala wao , Umri uliwatupa mkono na nguvu kuwaishia , hivyo vijana wenye uchu wa madaraka hawakusita kuwapindua na kufanikiwa kwa asilimia Mia  .

BOB JUNIOR Ni Nani ?
BOB JUNIOR ni mtoto wa simba maarufu aitwaye BOB MARLEY ambaye naye alishafariki muda mrefu huko nyuma na ndipo akaitwa BOB JUNIOR ( yaani BOB MARLEY mdogo ) . Pia alikuwa na kaka yake aliyetambulika kama Tryggve. 
Yaani mtu na kaka yake walikuwa wanatawala pamoja . BOB JUNIOR anatambuliwa sana kwa rangi yake nzuri na mvuto wake huku akivutia watalii wengi .
Mnamo Jumamosi tarehe 11 . 03 . 2023 Mfalme huyo aliyezeeka  alishambuliwa na simba vijana watatu ambao ni maadui zake  na kufariki , hakuwezi kuwahimili kutokana na uzee wake .
MAISHA YA SIMBA 
Simba ni moja wapo ya wanyama wanaoishi kwa makundi ambayo huitwa PRIDE ( Eneo lao la utawala )
Kundi hilo huundwa na wanaume kati ya  mmoja mpaka wanne , majike kadhaa na watoto wengi .

Simba wa kike hukaa kwenye hilo kundi mpaka wanazeeka na kufa ( yaani maisha yao yote ) ila simba wa kiume wanapofikisha miaka miwili mpaka minne huondoka kwenye kundi hilo aidha kwa kufukuzwa na Baba yao au huamua kuondoka wenyewe na huvamia kundi lingine na kutawala eneo hilo , yaani ni kama mapinduzi vile , kiongozi wa ufalme wako unapokuwa dhaifu wanakuja kukushambulia .

Kila simba ambaye ni kiongozi wa kundi huweka mipaka kwenye utawala wake kwa kutumia mkojo wake na pia huunguruma zaidi muda wa jioni na usiku ili kuzuia wavamizi wasiingie kwenye himaya yake .
Simba anapovamia himaya ya simba mwingine na kumuua pia huwaua na simba watoto wa kiume ili kutaka watoto wote wa kiume wawe damu yake 
Simba wa kike ndiyo wawindaji wakuu wa wanyama na siku zote hushirikiana kwa pamoja kwenye mawindo yao .

Hayo ndiyo maisha halisi ya Simba . Yaani Mwenye Nguvu ndiye mtawala .
Una maoni gani kuhusu Maisha ya Wafalme hawa wa Msitu ?

Source : National Geographics 
                BBC 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form