Mazoezi ni msingi mkubwa wa afya bora na kwenye miaka ya hivi karibuni hasa katika bara la Afrika kumekuwa na hamasa na uelewa mkubwa sana wa kufanya mazoezi , ndiyo maana kila uchao utasikia wanatangaza Marathon , leo mkoa huu kesho mkoa ule . Hata ukiingia status utakuta watu wanatupia picha wapo gym , bila ya kusahau vikundi mbalimbali vya kukimbia ( jogging ) , yaani kwa sasa kufanya mazoezi ndiyo fashion yenyewe . Tukiacha hizo mbwembwe zote .
Je unajua faida za kufanya mazoezi ? Hasa push ups ambazo unaweza kuzifanya hata ukiwa chumbani kwako umetulia .
Watafiti wa Havard walifanya utafiti kwa Wazimamoto wapatao 1104 wenye afya nzuri na wastani wa umri wao ulikuwa ni miaka 40 .
Kila mmoja aliambiwa apige push up nyingi kadri awezavyo na idadi ya push up hizo zilirekodiwa kwa kila mmoja . Baada ya miaka 10 , yaani kuanzia mwaka 2000 mpaka 2010 . Watafiti hao walikuja kugundua kuwa wale waliopiga push up nyingi zaidi walikuwa na uwezekano mdogo wa kupata magonjwa ya moyo .
Watafiti hao walipata majibu kuwa Wale walioweza kupiga push up 40 au zaidi kwa mara moja walikuwa na 96% ya uwezekano mdogo wa kupata magonjwa ya moyo ukilinganisha na wale waliopiga push up 10 au chini ya hapo .
" Utafiti huu unaonesha umuhimu wa mazoezi kwa afya , lakini haimaanishi kuwa ukishindwa kupiga push up 10 utapata Magonjwa ya moyo na pia ukiweza kupiga push up 40 hautapata Magonjwa ya moyo , kwani kuna sababu ( factors ) nyingine zinachangia kupata Magonjwa ya moyo pia " Dr Stafano N Kales , Havard.
Chanzo : Havard School Of Public Health