Msimu wa pili wa Series maarufu ya THE NIGHT AGENT ya Netflix utaachiwa mnamo mwaka 2024 .Msimu wa kwanza wa series hiyo uliachiwa mnamo tarehe 23 . 03 . 2023 Na kwa wiki yake ya kwanza [ tarehe 20 - 26 Mwezi Wa Tatu] kwenye tovuti ya Netflix imetazamwa kwa zaidi ya masaa 168,710,000 [ Masaa Milioni 168.7 ] .
Series hiyo inamuhusu Afisa wa shirika la upelelezi la FBI anapewa kazi ya kupokea simu za maafisa upelelezi wa siri ndani ya ikulu ya Marekani ( WHITE HOUSE ) . Simu hiyo haikuwahi kuita kwa muda mrefu na hatimaye siku moja simu hiyo inaita na baada ya kupokea simu hiyo anajikuta yupo katikati ya Njama nzito zenye siri zilizojificha za taifa hilo na uhalifu wa hali ya juu ambacho unahusu kutaka kumuua Raisi wa Marekani. Na afisa huyo anajikuta uhai wake ukiwa rehani huku akiwindwa na wauaji hatari
Tags
Movies