Je Unafahamu Kuhusu Kisiwa Cha Watu Wanaoishi Miaka Mingi Kuliko Wote Duniani ?

Je Ushawahi kukutana au kusikia kuhusu mtu mwenye miaka Mia moja au zaidi katika jamii yako .

Wakati unafikiria na kuvuta kumbukumbu basi nikujulishe kuwa kwenye nchi ya Japani kuna zaidi ya Wazee 70,000 wenye umri wa miaka Mia na zaidi . Usishangae sana , ndiyo kwanza tunaanza . Sasa katika kijiji cha Ogimi , kilichopo kwenye Kisiwa cha Okinawa huko kusini mwa Japani .Kwa mwaka 2020 kulikuwa na takribani wazee 15 wenye miaka 100 au zaidi kwa wakazi 3000 wa kijiji hicho.

Wakati tunajiandaa ili nikupeleke kwenye kijiji hicho cha Ogimi , wakati tunaingia kwenye kijiji hicho utaona jiwe dogo ambalo limeandikwa maneno ya kijapani yanayosomeka " Ukiwa na miaka 80 bado ni kijana mdogo sana , Unapofika miaka 90 na ancestors( mababu , wakongwe ) wako wakija kukutaka uende mbinguni ( kufa ) Waambie kuwa wasubiri mpaka ufike miaka 100 na hapo ndipo utaweza kufikiria ombi lao " .

Jiwe Lenye Maneno hayo 

Kisiwa cha Okinawa ni moja ya maeneo matano duniani yanayoitwa BLUE ZONES ambayo yanaongoza kwa watu wenye umri mrefu na watu wake wanafuraha na afya njema zaidi. Maeneo mengine manne ni Sardinia, Italy; Nicoya, Costa Rica; Ikaria, Greece; na Loma Linda, California .

Inasemekana kuwa 67% ya kuishi umri mrefu wa watu wa Okinawa ni Mlo wao pamoja na Mtindo wao wa maisha na huku 33% inatokana na vinasaba ( genetics ) .Kwenye makala hii tutazungumzia kuhusu Mlo wa watu wa Okinawa(diet ) pamoja na Mtindo wao wa maisha ( lifestyle ).

Vyakula Vyao .

1 . Watu Wa Kijiji Hicho Hula Mchanganyiko wa Vyakula takribani 206 Na Mara nyingi huwa ni mbogamboga .Na Kwa siku Hula takribani aina 18 za vyakula hivyo .Vyakula hivyo mbalimbali huwiweka kwenye visahani vidovidogo ( vijana wanaita mboga saba au drafti ) .

Mojawapo ya vyakula vinavyoliwa sana Okinawa ni :

Tofu 

Miso 

Tuna 

Carrots 

Goya (bitter melon) 

Kombu (sea kelp) 

Cabbage 

Nori (seaweed) 

Onion 

Soy sprouts 

Hechima (cucumber-like gourd) 

Soybeans (boiled or raw) 

Sweet potato ( viazi vitamu )

Peppers 

Sanpin-cha (jasmine tea).


Vyakula vya hapo juu huliwa Maranyingi sana kwenye jamii hiyo na vinatambuliwa kwa kuwa na antioxidants nyingi ( kuimarisha seli za mwili na kupambana na maradhi mbalimbali )

2 . Watu hao pia Hula takribani milo mitano ya Matunda Na Mbogamboga mbalimbali kwa siku .Huku 30% ya kalori zao kwa siku hutokana na Mbogamboga. ( mboga nyingi chakula kidogo )

3 .Hula Nafaka kula siku na mahususi ni Mchele .Hupendelea kula wali .

4 . Hula sukari Mara chache sana na hupendelea sukari inayotokana na muwa .pia hunywa sana juisi ya miwa .

Pia watu wa Okinawa wana utaratibu wa kula chakula kwa asilimia 80 tuu . Yaani unaacha kula pale unapohisi unakaribia kushiba . Watu wa Okinawa hawali chakula kingi sana . yaani wanadhibiti kiwango cha vyakuka vya nishati ( wanga na mafuta )[ calorie restriction ] .

Baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa Calorie Restrictions ni muhimu sana kwa kuwa 

1 . Inapunguza kiwango cha kemikali ya IGF 1 ambayo inahusishwa na kuzeeka [ seli kufa haraka na mapema ] na inflammation. 

2 . Inapunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama Kisukari , Uzito Uliopitiliza [ Obesity ] , Pressure , Magonjwa ya Moyo, Inflammation Na Kupunguza hatari ya kupata saratani .Watu wa Okinawa huwa chakula kidogo ila chenye virutubisho vingi na vya kutosha.

Mtindo wa maisha yao .

Unapofika Okinawa utaona wazee wakifanya shughuli mbalimbali za kawaida kwenye jamii yao na huongozwa na mtindo wa maisha unaoitwa IKGAI ( kuishi kwa lengo lako lililokuleta duniani na kutoacha kufanya kazi mpaka unakufa )Watu wa Okinawa siku zote huwa wanafanya shughuli ndogo ndogo [ stay active ] .

Hata wazee wa miaka zaidi ya 90 nao pia hufanya shughuli mbalimbali. Watu wa Okinawa huamka asubuhi na mapema na kufanya mazoezi mepesi ya viungo ysitwayo RADIO TAIDO , Kisha Wanatembea kwa muda mrefu , hupenda kuimba karaoke na majirani zao na pia hupendelea kutunza bustani zao .Shughuli zote hizo huwafanya kuwa active sana .

Tafiti zilizofanywa zinaonesha kuwa kukaa kwa takribani masaa 6 mpaka 8 kwa siku bila ya kupata takribani dakika 20 za kutembea huweza kuongezeza uwezekano wa 10% mpaka 20% ya kupata maradhi ya Moyo Na Uzito Uliopitiliza.

Pia jamii huwa na ushirikiano mkubwaHata pale inapotokea mmoja wao ana tatizo , huwa naye pamoja na kuibeba changamoto hiyo kama ya jamii nzima . Hii hufanya watu wa Okinawa kutokuwa na msongo mkubwa wa mawazo ( stress ) .Wataalamu wamethibitisha kuwa Stress hupelekea seli kuzeeka haraka na kuleta vifo vya mapema.


Basi hayo ndiyo maisha ya wakazi wa kijiji cha Ogimi kilichopo kisiwa cha Okinawa ambao wanajulikana kwa kuwa na umri mkubwa.  Je umejifunza nini kupitia maisha ya watu wa Okinawa?

Sources : National Geographics 

                   BBC Travel 

                    IKIGAI by Francesc Miralles na  Hector Garcia

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form