Mashindano ya vilabu vya Afrika yanatamatika rasmi mwezi huu wa sita ( June ) huku Mashindano ya Shirikisho [ CAF CONFEDERATION CUP ] tayari yameisha tarehe 03 . 06 . 2023 kwa USM Alger kuchukua kombe mbele ya Timu pekee kutoka Afrika Mashariki na Tanzania kwa ujumla , yaani Young Africans . Upande wa klabu bingwa Afrika [ CAF CHAMPIONS LEAGUE ] mchezo wa kwanza utachezwa leo tarehe 04 . 06 . 2023 kati ya Wydad Casablanca Dhidi ya Al Ahly na fainali ya pili itakuwa 11 . 06 . 2023 .
Baada ya kutamatika kwa Mashindano hayo, CAF huzipa kila timu Alama kulingana na viwango vilivyooneshwa na timu husika . Kwa msimu wa 2022 - 2023 . Viwango vya timu na alama zao ni kama zifuatazo, huku kukuwa na ingizo jipya la timu ya Young Africans ndani ya orodha ya timu hizo 20 ;
1 . Al-Ahly [ Misri ] = 78
2 . Wydad AC [ Morocco ] = 74
3 . Espérance de Tunis [ Tunisia ] = 56
4 . Mamelodi Sundowns [ Afrika Kusini ] = 51
5 . Raja Casablanca [ Morocco ] = 51
6 . Zamalek [ Misri ] = 39
7 . RS Berkane [ Morocco ] = 37
8 . CR Belouizdad [ Algeria ] = 36
9 . Simba [ Tanzania ] = 35
10 . Pyramids [ Misri ] = 35
11 . Petro de Luanda [ Angola ] = 33.5
12 . JS Kabylie [ Algeria ] = 31
13 . TP Mazembe [ DR Congo ] = 30.5
14 . Horoya [ Guinea ] = 29
15 . USM Alger [ Algeria ] = 27
16 . Orlando Pirates [ Afrika Kusini ] = 24
17 . Al-Hilal [ Sudan ] = 23
18 . Young Africans [ Tanzania ] = 20
19 . ASEC Mimosas [ Ivory Coast ] = 20
20 . Étoile du Sahel [ Tunisia ] 20 .
NB : Alama za Al Ahly Na Wydad Casablanca zitabadilika kutokana na mchezo wa fainali ya pili kukamilika ...
Alama [ Points ] za Timu Klabu bingwa [ CAF CHAMPIONS LEAGUE ] :
Bingwa = 6
Mshindi wa pili = 5
Nusu fainali = 4
Robo fainali = 3
Nafasi ya 3 hatua ya makundi = 2
Nafasi ya 4 hatua ya makundi = 1 .
Alama [ Points ] za Timu Kombe La Shirikisho [ CAF CONFEDERATION CUP ] .
Bingwa = 5
Mshindi wa pili = 4
Nusu fainali = 3
Robo fainali = 2
Nafasi ya 3 hatua ya makundi = 1
Nafasi ya 4 hatua ya makundi = 0.5
Alama zinavyogawanywa :
2022 - 2023 = Alama za timu × 5
2021 - 2022 = Alama za timu × 4
2020 - 2021 = Alama za timu × 3
2019 - 2020 = Alama za timu × 2
2018 - 2019 = Alama za timu × 1 ...
Alama 35 za Simba :
2018 - 2019 : 3 × 1 = 3
2019 - 2020 : 0 × 2 = 0
2020 - 2021 : 3 × 3 = 9
2021 - 2022 : 2 × 4 = 8
2022 - 2023 : 3 × 5 = 15
Jumla : 3+9+8+15 = 35
Alama 20 za Yanga
2018 - 2019 : 0 × 1 = 0
2019 - 2020 : 0 × 2 = 0
2020 - 2021 : 0 × 3 = 0
2021 - 2022 : 0 × 4 = 0
2022 - 2023 : 4 × 5 = 20
Jumla ya Alama : 20 .
Alama hizi hukusanywa kwa kipindi cha miaka mitano [ 5 ] na mfumo huu ulianzishwa rasmi na CAF mwaka 2017.