Kisa cha watu wa Pompeii walioangamizwa kwa mlipuko mkubwa wa volkano kutokana na uovu wao ni moja ya kisa maarufu sana duniani na kilichotajwa kwa wingi toka kwenye kurasa za vitabu mbalimbali vya kihistoria.Kihistoria Pompeii ulikuwa ni mji wa Roma ya kale uliopo Italia karibu na mji wa Napoli ya sasa.Katika mji wa Pompeii kulikuwa na uwanja mkubwa sana ulioweza kutosha watu wote wa mji huo,uwanja huo ulikuwa ukitumika kwa shughuli za maonesho ya kivita na mapambano ya watumwa pia ulitumika kwa starehe mbalimbali na maovu mengi yalikuwa yakifanyika kama vile ukahaba,ulevi,michezo ya kamari na mengine mengi.
Matajiri wengi wa Roma na wengine kutoka sehemu mbalimbali za miji mingine walipenda sana kwenda kwenye uwanja huo kwa starehe hizo.Karibu na mji wa Pompeii kulikuwa na mlima mkubwa uitwao Vesuvius ambao ulikuwa ni mlima wa volkano iliyokuwa ikichemka kwa muda wote huo,lakini watu wa Pompeii waliokuwa chini ya mlima huo walikuwa wakipuuza jambo hilo na kuendeleza maovu yao licha ya kuwa na dalilli zote za hatari ya kulipuka kwa volkano hiyo.
Na marakadhaa matetemeko ya ardhi yalibomoa baadhi ya nyumba zao kutokana na mitikisiko ya volkano hiyo.Ndipo mnamo usiku wa Tarehe 24 Augost 79BC volkano hiyo ikalipuka,lilikuwa ni janga kubwa mno kwasababu vumbi la moto wa volkano liliufunika mji mzima na kuangamiza watu wote waliokuwa hawajahama bado katika mji huo.Na baada ya karne nyingi kupita ndipo serikali ya Italia ilipoamua kuufukua mji huo na kukuta mabaki ya vitu vingi ikiwemo miili ya watu iliyokauka kwa kuungua na volkano hiyo huku ikiwa imekaa katika namna mbalimali kulingana na hali ya kifo ilivyoikuta.
Baadhi ya miili ilionekana kuwa ni kama ilikuwa imelala kitandani na mingine ilikuwa imekaa katika hali mbalimbali za kufanya uovu.Mpaka sasa sehemu hiyo imebakia kama sehemu ya makumbusho ya kihistoria.
Video Clip 👇