STRANGER THINGS ILIKATALIWA ZAIDI YA MARA 15

 

STRANGER THINGS ni Series ya kutisha ya kisayansi ( science fiction horror series ) inayohusu kutokea kwa viumbe wa ajabu kutoka kwenye dunia nyingine inayofanana na yetu . Viumbe hao wameingia kwenye mji wa Hawkins baada ya geti linalotenganisha na dunia yetu kufunguka na kuleta hali ya sintofahamu duniani .

Yafuatayo ni mambo 7 muhimu ambavyo unapaswa kufahamu kuhusu series hii : 

1 . Series  hii ilianza kuonyeshw rasmi na tovuti ya Netflix Mnamo mwaka 2016 .Mandhari ya mazingira ya Tamthilia hii ni ya miaka ya 1980s kwenye Mji wa Hawkins huko Marekani 

2 . Stranger Things Imeanzishwa na kutengenezwa na Mapacha wawili ambao ni Matt Na Ross Duffer ( Duffer Brothers ) .

3 . The Duffer Brothers Waliipeleka na kutaka ionyeshwe kwenye Cables TV zaidi ya 15 Lakini TV hizo zote ziliikataa kwa kusema kuwa ina mambo mengi ya kitoto hivyo isingeuza sana . Hivyo wakawaambia kuwa watengeneze Tamthilia ya kitoto au Wangetoa wale watoto kwenye upelelezi wa Hoppers .

4 . Mnamo mwaka 2015 Kampuni ya 21 LAPS ENTERTAINMENT walinunua haki za kuzalisha Tamthilia hiyo baada ya kusoma na kuipenda stori hiyo .

5 . Mara ya Kwanza kabisa Mfululizo wa televisheni huu uliitwa MONTAUK . Hii ilitokana na Tamthilia hii kutengenezwa kwenye Mji wa MONTAUK , NEW YORK Ambao unahusishwa na Siri nyingi za kiserikali na Majaribio mbalimbali ya siri ya kisayansi .Baada ya kubadilishwa na kufanyia marekebisho stori hiyo , wakabadilisha Jina la Tamthilia na kuitwa STRANGER THINGS .

6 . Kuhusu kuandika maisha ya Mike Pamoja na rafiki zake . THE DUFFER BROTHERS Waliandika uhusika kulingana na maisha yao ya shule ya juu ( High School ) Kwani Nao waliishi kwa kutengwa na kivyao vyao

7 . Kipande cha mwisho cha season 3 episode ya 9 Ambapo kinaonesha Lucas Na Max wakipigana mabusu hakikuwa kimepangwa kwenye script na Walijulishwa siku moja kabla ya Kuigiza kwa kipande hicho .Cha kufurahisha zaidi ni kuwa wote yaani Sink ( MAX ) Pamoja na McLaughlin ( LUCAS ) Hawakuwahi kupiga mabusu mtu yeyote kwenye Maisha yao ya kawaida . Yaani aani busu Lao la kwanza maishani mwao lilipatikana kwenye kipande hicho cha Tamthilia ya STRANGER THINGS . ( 🖊 Luqman Kisokora )

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form